Jumatano, 9 Aprili 2014

MSANII GODFREY TUMAINI "DUDUBAYA" AFANYA UKATILI WA KUMKATA MAMA YAKE SIKIO BAADA YA KUMTUHUMU NI MCHAWI.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva Gdofrey Tumaini akijulikana kwa jina la kisanii kama DUDU BAYA anakabiliwa na kesi ya kujeruhi kwa kasu baada ya kutuhumiwa kumkata sikio mama yake mkubwa kwa kumtuhumu kwamba ni mchawi na ndio anaesababisha yeye kukwama kwenye mambo yake.

Akizungumza toka Mwanza na kituo cha redio cha Clouds Fm katika kipindi cha burudani cha XXL mdogo wa msanii huyo anaejulikana kwa jina la Mueta Tumaini alikiri kutokea kwa tukio hilo la kinyama kwa mama  yao mkubwa  lililofanywa na kaka yake na kuthibitisha kwamba wamesharipoti polisi na kaka yake huyo anatafutwa kwa kutuhumiwa kufanya unyama huo.

Mueta alisema kwamba alipigiwa simu na mama yao mzazi kumpa taarifa hizo kwamba kaka yake yaani Dudubaya amemkata sikio mama yao mkubwa kwa tuhuma kwamba ni mchawi. 

"Nilipigiwa simu na Mama akinambia kwamba watoto wa mama mkubwa wamepigia simu kwamba Godfrey (Dudubaya) amekwenda nyumbani kwa Mama mkubwa ambae na kutenda unyama wa kumkata sikio huku sababu kubwa ni tuhuma za uchawi ambazo Dudubaya amekuwa akimtuhumu Mama mkubwa huyo" alisema Mueta.

Mueta aliendea kusema kwamba "baada ya kumuuliza Mama mkubwa sababu za kukatwa sikio alinambia kwamba kaka anadai kwamba anamroga na amekuja kutekeleza azma yake hiyo, lakini ukiangalia sababu hiyo sio ya msingi kabisa na hakuna uthibitisho juu ya hilo".

Dudu alipofika pale alimuita mama yake mkubwa na hakuitikiwa ndipo alipomkokota mama yake mkubwa kutoka kibarazani nje na kumuingiza ndani sebuleni akamlaza kwenye kochi na kuanza kumkata sikio lakini hakufanikiwa kuling'oa lote kwasababu mama mkubwa alipiga kelele kuita majirani ndipo Dudubaya akatoka nje na kutokomea kusikojulikana, lakini wakati Dudu anafanya yote hayo mule ndani alikuwepo mtoto mmoja mdogo ambaye hakuweza kumzuia mjomba wake asifanye ukatili huo, 

 Majirani wakafika na kutoa msaada wa kwanza kwa bi Mkubwa na kumwahisha Hospitali ya Sekeu Toure akashonwa sikio, kwani sikio hilo halikukatika kabisa kwa sababu kisu alichokua anatumia Dudubaya kilikua butu.

Sikiliza kisa kamili hapa chini. 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni