Jumanne, 25 Machi 2014

TAMKO LA MUUNGANO WA WASICHANA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI TAREHE 08.03.2012.

Mwenyekiti
 
Ndugu Mgeni Rasmi,

Awali ya yote naomba nichukue fursa kuwashukuru wasichana viongozi  kwa kuandaa jumuiko hili katika siku hii muhimu ya kuadhimisha Miaka 101 ya Siku ya Wanawake Duniani. Siku ya wanawake duniani imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kuenzi, kupongeza na kuwapa moyo wanawake wote  duniani kwa mchango wao waliotoa na wanaoendelea kutoa katika sekta ya siasa, uchumi na kijamii ili kuleta maendeleo duniani.

Ndugu Mgeni Rasmi, tunakushukuru wewe binafsi kwa kujumuika nasi  katika kutafakari kwa undani mafanikio na changamoto mbalimbali zinazowakabili wasichana katika kuleta maendeleo yetu na jamii kwa ujumla.Pia shukrani nyingi ziwaendee  washiriki wote wa kusanyiko hili ambao  
tunachukia  na  kulaani vitendo vya ukatili dhidi  ya wasichana na watoto.  
 Ndugu mgeni rasmi,wimbi  hili  la utafiti uliofanywa na UNIAS vijana kati ya umri wa miaka 15-20 walioambukizwa na ukimwi theluthi mbili ni wasichana katika baadhi ya maeneo ya Afrika wasichana wapo hatarini kuambukizwa vvu mara sita zaidi ya vijana wa kiume.     
Utafiti unaonesha kuwa duniani kote wasichana zaidi ya miambili wanasafirishwa kwa njia haramu kila mwaka na walio wengi  wanakuwa hatarini katika kufanyiwa ukatili wa kingono na kuambukizwa vvu.
Ukatili wa kingono unatendeka kwa kiwango cha juu sana Tanzania asilimia 40.4% ya wasichana tendo la kujamiiana kwa mara ya kwanza  limefanyika kwa njia ya kubakwa(Garcia Moreno).
Ndugu Mgeni Rasmi,kutokana na hali ya vitendo vya ukatili dhidi ya wasichana kuwa mbaya tunaomba kuwakumbusha na kuiomba serikali,wadau,vikundi visivyo vya kiserikali,viongozi wa dini na jamii  kutoa elimu juu ya kumuwezesha mtoto wa kike.Mfano:kutoa elimu juu ya kujikinga na ubakaji,(self defense mechanism) ushilikishwaji katika ngazi ya kutoa maamuzi.kupitia elimu hii itapunguza ukatili na vitendo vinavyo bagua wasichana na pia wasichana watapata fursa ya kushiriki katika kutoa maoni/mawazo na kuchochea maendeleo katika nchi yetu ya Tanzania.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                
Ndugu mgeni rasmi, kivulini  ni shirika linalojishughulisha  na shughuli  za kijaamii kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kupitia kampeni ya tunaweza tumeona  jamii imeelewa nini maana ya ukatili nahivyo kupunguza ukatili dhidi ya wasichana na watoto.Kampeni hii imeweza kubadili mitazamo hasi ya  wanajamii dhidi ya wasichana na kuwa wanamabadiliko walioacha vitendo vya ukatili, wanamabadiliko hao wameanza kujitolea kuwashawishi watu wengine kubadili mienendo na tabia zao.

Ushiriki hafifu wa wasichana katika mambo mbalimbali kuanzia ngazi ya familia, jamii na nchi kwa ujumla umekuwa ni changamoto kutokana na;
·        Mila, desturi na tamaduni potofu zinazo mkandamiza msichana zimekuwa zikiendelezwa na wanajamii na hivyo kushusha thamani ya msichana katika jamii.
·        Kutoshiriki na kutoshirikishwa kwa wasichana katika shughuli za maendeleo
·        Uoga, aibu na kutojiamini kwa wasichana kwamba wanaweza
Hali hii imekuwa ni kipingamizi kikubwa katika harakati za maendeleo katika jamii yetu. Kupitia kauli mbiu ya mwaka huu USHIRIKI WA WASICHANA UNACHOCHEA MAENDELEO, tunapenda kuiomba jamii na wadau wote wa maendeleo kuwashirikisha na kuwaelimisha wasichana kuhusiana na umuhimu wao katika shughuli za maendeleo kwani UKIMUELIMISHA MSICHANA UMEIELIMISHA JAMII NZIMA
Ndugu Mgeni Rasmi,kutokana na hali ya vitendo vya ukatili dhidi ya wasichana kuwa mbaya tunaomba kuwakumbusha na kuiomba serikali,wadau,vikundi visivyo vya kiserikali,viongozi wa dini na jamii   juu ya kumuwezesha mtoto wa kike.Mfano:kutoa elimu juu ya kujikinga na ubakaji,(self defese mechanism) ushilikishwaji katika ngazi ya kutoa maamuzi.kupitia elimu hii itapunguza ukatili na vitendo vinavyo bagua wasichana na pia wasichana watapata fursa ya kushiriki katika kutoa maoni/mawazo na kuchochea maendeleo katika nchi yetu ya Tanzania.
                                                                                                                                                                                                                                                                                                                               
Mapendekezo/Maoni:
 Ndugu Mgeni Rasmi, kupitia muungano wa Wasichana jijini Mwanza ili kuweza kuongeza ushiriki wa wasichana katika shughuli mbalimbali zenye kuchochea maendeleo, tunaomba;
·        Serikali ianzishe mahakama maalumu zitakazo shughulikia kesi za ukatili dhidi ya wasichana kwani uwepo wa dawati la jamii pekee katika mahakama na vituo vya polisi haitoshi.
·        Serikali Kuu kupitia Serikali za mitaa, zitenge fungu maalum la pesa ambazo zitatumika kutoa elimu kwa wasichana juu ya uongozi na nafasi yao katika jamii.
·        Serikali kupitia sekta ya elimu, isisitize ufundishwaji wa mada zinazohusiana na uongozi, nafasi ya wasichana na ushiriki wao katika jamii, kupitia somo la Uraia na Stadi za kazi.
·        Viongozi wa dini, mashirika yasiyo ya kiserikali na wanahabari wapinge na kuzuia mila na desturi potofu zinazombagua msichana kushiriki katika shughuli zenye kuletea maendeleo ya jamii yetu.
·        Serikali kupitia wanahabari, tutengewe vipindi maalumu vya redio na runinga, pia ukurasa maalum katika magazeti pendwa ili kuweza kuwaelimisha na kuwajengea uwezo wasichana katika maswala mbalimbali.
·        Wazazi na jamii watoe taarifa za vitendo vya ukatili sehemu husika ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wale wote wanaotenda vitendo hivyo .
·        Watoa huduma ya afya (madaktari na wauguzi) Tunaomba kuwahudumia wasichana wote waliofanyiwa vitendo vya ukatili  mfano; kubakwa, kupigwa na kujeruhiwa wanaopelekwa katika hospitali na vituo vya afya pasipo kuangalia malipo kwanza.
·        Wasichana kushiriki kwa ukaribu katika shughuli zote kuanzia ngazi ya familia, jamii na nchi pasipo kungoja washirikishwe. Kwani ni wajibu wao kushiriki.
·        Wasichana  tunatakiwa kuondoa aibu, uoga na mitazamo potofu dhidi yetu kwamba hatuwawezi kufanya chochote.

Ndugu Mgeni Rasmi,
Mwanamke aliye shinda tuzo ya kuwa mwanamke jasiri Jijini Mwanza mwaka 2011 (Mama Maimuna Kanyamala), hupenda kusema kwamba:
KUMWEZESHA NA KUMSHIRIKISHA MTOTO WA KIKE NI KUMUANDAA KUWA KIONGOZI BORA, SHUPAVU NA JASIRI WA  SASA NA BAADAE.
WASICHANA TUKIWEZESHWA TUNAWEZA  TUSHILIKISHANE NA TUSAIDIANE KATIKA KULETA MAENDELEO.

Asanteni,

Lilian Richard
Katibu, Young Women Leadership
Mwanza.                                                    

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni