 |
Mkurugenzi
wa Shirika la KIVULINI Bw. Ramadhan Masele akizungumza na Wasaidizi wa Kisheria
(hawapo pichani) wilaya ya Sengerema cha tathmini ya utendaji kazi wa Wasaidizi
wa kisheria chini ya mradi wa msaada wa kisheria na haki za binaadamu kilichoanza
mapema asubuhi.
|
 |
| Baadhi
ya wasaidizi wa kisheria katika wilaya ya Sengerema wakiwa katika kikao cha
tathmini ya utendaji kazi wao kwa kipindi cha robo ya pili ya Mwaka kwa mradi
wa mradi wa msaada wa kisheria na haki
za binaadamu. |
 |
| Bi
Eunice Mayengela Mwanasheria toka Shirika la KIVULINI akitoa ripoti ya utendaji
kazi wa Mradi wa msaada wa kisheria na haki za binaadamu kwa washiriki. Bi.
Eunice alisema kuwa Lengo la umoja wa Wasaidizi wa kisheria ni
kuhakikisha unasimamia shuguli zote za msaada wa kisheria katika wilaya husika,
na ni kiunganishi cha wasidizi wa kisheria katika ngazi ya wilaya. |
 |
| Bi Eunice Mayongela akisisitiza jambo kuhusu Mkutao
wa siku moja ulifanyika katika wilaya ya sengerema kwa lengo la kuzungumzia maendeleo ya mradi na changamoto zinaojitokeza. |
 |
Mkurugenzi
wa Shirika la KIVULINI akisisitiza Katika kipindi hiki Kivulini iliweza
kutengeneza vitabu kwa ajili ya kuandikishia shauri, kutolea rufaa ,na kupata
mrejesho wa rufaa kutoka kwa watoa huduma wengine na kugawanywa kwa wasidizi wa
kisheria, Pia Kivulini iliweza kuwatengenezea vitambulisho wasidizi wa kisheria
ili waweze kutambulikana kwa urahisi Zaidi katika jamii zao.
|
 |
| Baadhi ya Wasaidizi wa Kisheria toka wilaya ya
Sengerema wakisikiliza kwa makini ripoti ya kiutendaji katika wilaya ya
Sengerema, Mwanza. |
Sengerema, Mwanza.
Taasisi
isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na kutetea haki za Wanawake, KIVULINI,
yenye makao makuu jijini Mwanza imeanza kufanya vikao vya tathmini ya utendeji
kazi wa wasaidizi wa kisheria kwa robo mwaka ya pili katika ngazi za wilaya
chini ya mradi wa msaada wa kisheria na haki za binaadamu.
Vikao
hivyo vilivyoanza leo katika wilaya ya Sengerema kwa kukutana na wasaidizi wa
kisheria 25 wanaofanya kazi ya kutatua migogoro ya kisheria katika vijiniwilaya
ya sengerema huku vikao hovyo vinatarajiwa kufanyika pia katika wilaya ya Magu,
Misungwi na Kwimba zote zipo ndani ya mkoa wa Mwanza.
Kivulini kupitia mradi wa msaada wa kisheria imetekeleza shughuli
mbalimbali kwa lengo la kuisaidia jamii kupata uelewa wa haki zao za kisheria
na pia kundeleza uwepo wa elimu na ushauri wa kisheria katika maeneo ambayo
mradi unatekelezwa.
Na juhudi kubwa imewekwa katika kuwajengea uwezo wasaidizi wa kisheria
kwasabaabu wasidizi wa kisheria wanaitajika ili kuiwezesha jamii kuweza kupata
haki hasa wale walioko pembezoni.Na kwa kupitia umoja wa wasaidizi wa kisheria
wataweza kutoa elimu kwa wanajamii ili waweze kujua haki zo za kisheria .na
matatizo yanayopelekea uvunjifu wa haki na kuchukua hatua.
Kivulini Iliwezesha
uundwaji wa umoja wa vikundi vinne vya wasaidizi wa kisheria ktika wilaya ya kwimba,Misungwi,Sengerema,Na
Magu na umoja huo unaundwa na jumla ya
wajumbe 25 kila kikundi ambao walipata mafunzo ya wasaidizi wa kisheria kwa
kutumia mtaala wa chama cha wanasheria Tanganyika.
Wasaidizi wa
kisheria wameendelea kutoa huduma ya ushauri wa kisheria kwa wanajamii hasa kwa makundi yasiyojiweza katika kata 52,
kwa kipindi cha robo mwaka ya pili wasaidizi wa kisheria wamepokea mashauri 129
kwa ujumla katika mashauri hayo yaliyokamilika ni mashauri 60 yaliyotolewa
rufaa ni 43 na yanayoendelea nimashauri 43, ukilinganisha na robo mwaka ya
kwanza ambapo mashauri 200 yalipokelewa ambayo inafanya jumla ya mashauri 329
yaliyopokelewa na wasaidizi wa kisheria.